KUHUSU SISI

Karibu G-A Nutrition – Lishe Asilia kwa Maisha Yenye Afya na Matokeo ya Kweli

Mimi ni Meshack Mwandampapa, mwanzilishi wa G-A Nutrition. Nilianzisha kampuni hii kutokana na uzoefu wangu binafsi wa kupambana na changamoto mbalimbali za kiafya kama mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, uchovu, maumivu ya viungo, macho, miguu kuwaka moto, mafua ya kila mara na kupungua kwa kinga mwilini.

Mwaka 2024, nilihamia Dar es Salaam kutafuta maisha kupitia biashara ya virutubisho katika mfumo wa network marketing. Katika harakati hizo, niligundua lishe ya asili iliyotengenezwa kwa mmea wa grain amaranth – mimea tajiri kwa virutubisho muhimu mwilini. Nilipoanza kuitumia, nilishuhudia mabadiliko makubwa kwa muda mfupi. Kwa mara ya kwanza, nilijihisi mwenye nguvu, huru kutokana na mafua, na mapigo ya moyo kurudi katika hali ya kawaida.

Uzoefu huo ulinipa hamasa ya kushirikisha wengine. Nilianza kuwapa watu wa karibu, waliokuwa na matatizo ya kisukari, presha, selimundu, na viungo – na wengi walirudi na ushuhuda wa kuboreka. Hapo ndipo wazo la G-A Nutrition lilizaliwa – jina lililotokana na kifupi cha Grain Amaranth, likiwa na azma ya kupeleka tiba hii ya asili kwa watu wengi zaidi.

Kupitia msaada wa wataalamu na mafunzo kutoka SIDO, G-A Nutrition imekua na kufuata taratibu zote za kiafya ili kutoa lishe salama, yenye ubora na matokeo halisi.

DIRA YETU

Kuona jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla ikipata nafuu ya kiafya kwa kutumia lishe asilia, salama na yenye matokeo ya haraka kwa gharama nafuu.

DHAMIRA YETU

Kutoa lishe ya ubora wa juu inayotokana na grain amaranth kwa watu wenye changamoto mbalimbali za kiafya, kwa lengo la kuimarisha afya zao kwa njia ya asili, kwa kuwahudumia kwa uaminifu, elimu, na matokeo yanayoshuhudiwa.

KAULI MBIU

"Kila kijiko kimebeba matokeo." "Lishe asilia, matokeo halisi."

MAADILI YA KAMPUNI

Ukweli na Uaminifu: Tunatoa taarifa sahihi, bila kupotosha wateja wetu. • 

Matokeo Yanayothibitishwa: Tunategemea ushuhuda halisi kutoka kwa wateja waliopata matokeo. Afya Kwanza: Kipaumbele chetu ni afya na ustawi wa mteja, si faida. Elimu kwa Jamii: Tunahakikisha kila mteja anaelewa vizuri faida za lishe anayopata. Ubunifu: Tunabuni njia bora zaidi za kusambaza lishe yenye ubora kwa urahisi.

MWANZILISHI WETU

Mr. Meshack Mwandampapa ni mwanzilishi wa G-A Nutrition. Baada ya kupambana na changamoto nyingi za kiafya, aligundua nguvu kubwa ya lishe ya asili inayotokana na mmea wa grain amaranth. Kupitia ushuhuda wa kweli kutoka kwake na watu wa karibu, aliweka msingi wa kampuni hii ili kuwasaidia watu wengi zaidi wapate afya kwa njia salama na ya asili. Leo hii, yeye ni mhamasishaji wa lishe asilia, mkufunzi na mtoa huduma za afya mbadala kupitia G-A Nutrition.




Post a Comment

0 Comments